https://www.youtube.com/watch?v=95VG8sS5pRQ
Viongozi wa muungano wa Jubilee kutoka maeneo ya Magharibi sasa wamemtaka kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula kuvunja ndoa yake ya kisiasa na kinara wa CORD Raila Odinga, wakidai upinzani hauna nafasi ya kuunda serikali katika uchaguzi mkuu ujao.
Wakiongozwa na waziri wa maji Eugene Wamalwa mjini Kitale, viongozi hawa wamesema Wetangula hana budi ila kuupiga teke muungano wa CORD, kwani tayari amekiri kwamba Odinga hana nafasi ya kuingia Ikulu. Wetangula anakariri habanduki ng'o, kutoka kwenye muungano huo.
The post Viiongozi wa magharibi wamrai Wetangula kuhama CORD appeared first on Mediamax Network Limited.