https://www.youtube.com/watch?v=oUj5vvg9ROw
Rais Uhuru Kenyatta ameelezea masikitiko yake kutokana na kile anachosema ni jaribio la viongozi kuhujumu katiba ya nchi, na kudunisha tume huru zilizoundwa chini ya katiba hiyo.
Akizungumza wakati akihitimisha ziara yake ya Kaskazini Mashariki mjini Garissa, Kenyatta amesema ni aibu kwa viongozi wanaojua kusoma na kuelewa katiba kujaribu kutumia kifua kuibandua tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, ilhali kuna njia za kisheria zilizowekwa.
The post Uhuru na Ruto waendelea kuusimanga upinzani huko Garissa appeared first on Mediamax Network Limited.