https://www.youtube.com/watch?v=ukJ9yTkpRy0
Kikao kinachochunguza sakata ya jaji Philip Tunoi na gavana wa Nairobi Evans Kidero kimeendelea leo, huku ikiibuka kwamba mshukiwa Geoffrey Kiplagat al maarufu Lelmet alijiwasilisha kwa maafisa wa polisi hususan makachero wa CID, akitaka wamsaidie apate malipo yake ya shillingi millioni 30 kutoka kwa jaji Tunoi na gavana Kidero.
Hata hivyo, polisi wamejitetea kuwa hawakumkamata Lelmet ingawa alikuwa akitaka pesa kwa njia isiyo halali wakisema kuwa walidhania yeye ndiye aliyepasua mbarika kuhusiana na sakata hiyo.
The post Sakata Ya Jaji Tunoi : Shahidi Kiplagat alitafuta usaidizi wa polisi alipwe Sh 30M appeared first on Mediamax Network Limited.