Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kali kwa mawaziri na makatibu kwamba kila mmoja atajibu lolote litakalotokea kwenye wizara wanazosimamia. Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa mawaziri saba na makatibu kumi na tisa wapya walioidhinishwa na bunge, Kenyatta amesema majukumu ya kila mmoja sasa yako wazi, hivyo basi hakuna atakaye mnyooshea mwenzake kidole cha lawama kuhusu shughuli katika wizara.. Kiama Kariuki anatuarifu.
The post Rais ashuhudia kuapishwa kwa mawaziri 7, makatibu 19 appeared first on Mediamax Network Limited.