https://www.youtube.com/watch?v=yka0gJZ3riw&feature=youtu.be
Baraza la kitaifa la mitihani KNEC limewahakikishia wanafunzi wanoendelea na mtihani wao wa KCSE kwamba zoezi la kuwatahini litaendelea hadi mwisho na hakuna nia yeyote ya kusitisha mtihani huo.
Haya yanajiri huku ujumbe wa KNEC ukizidi kukanganya wengi kwani hata baada ya kuthibitisha kuwa kuna visa ambavyo kwa sasa vinachunguzwa kutokana na madai ya kuwepo kwa udanganyifu na wizi wa mitihani bado KNEC inashikilia msimamo kwamba zoezi hilo limezingatia kanuni zilizowekwa na hadhi yake isitiliwe shaka.
Anders Ihachi bado anazamia utata unaozingira mtihani wa mwaka huu wa KCSE
The post Baraza la KNEC lakiri kuna udanganyifu lakini KCSE utaendelea appeared first on Mediamax Network Limited.