Hali hiyo imeendelea kuibua hisia miongoni mwa wananchi kaunti ya Mombasa, huku baadhi wakinyoshea kidole cha lawama kwa serikali.
Wengine wameonekana kutoridhishwa na hatua ya madaktari kushiriki katika mgomo wakisema kuna ulazima wa pande zote mbili kuafikia makubaliano ili kuokoa maisha ya wananchi wanaoathirika na mgomo huo.
Madaktari wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 22 wakiitaka serikali kuwapa nyongeza ya mshahara kwa asilimia 300, jambo ambalo limeonekana kugonga mwamba.
The post Mgomo wa madaktari waendelea kuibua hisia miongoni mwa wananchi appeared first on Mediamax Network Limited.