https://www.youtube.com/watch?v=OA60EYhn33I
Kampeni za mwanzo kwenye msukumo wa maandalizi kwa uchaguzi wa mwaka 2017 zinaonekana zimeanza ila tu wapinzani wakuu, CORD na Jubilee hawadhihirishi wazi kuwa ndoano zao zishajitokeza tayari kila upande kuvutia kwake.
Ziara za rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwenye ngome kuu za CORD zikiwa dhihirisho kuwa sasa ni kusaka kule walikoteleza hukuCORD nayo ikiwa na shinikizo la kusambaratisha mwelekeo wa mambo kwa kudokoa dokoa kwenye usimamizi wa uchaguzi kwa kudai kuwa tume ya IEBC ivunjiliwe mbali. Kwenye makala ya ya rhumba la siasa Anders Ihachi anachanganua mwelekeo wa kisiasa ulivyokuwa hasa kati ya CORD na Jubilee juma hili.
The post Rumba La Siasa : Mchakato wa CORD na Jubilee kugombania urais katika uchaguzi mkuu 2017 appeared first on Mediamax Network Limited.